Hii ni hadithi fupi kuhusu maisha ya mwanadamu, tokea kuzaliwa mpaka kuwa na akili timamu kwani imeonekana wanaume kuwafanyia vitendo vya ukatili wanawake hata kufikia kuwapotezea maisha. Kwa hakika ni kitendo cha aibu kwa mwanaume yeyote kufikia hatua ya kumkata mkewe kwa kutumia mapanga, hii imetokea sehem mbalimbali na hivi karibuni huko mwanga kilimanjaro kwa maisha ya kawaida ni aibu sana. Mwangalie huyo mama hapo pichani na niambie alivyo na mapenzi na mwanae, kumbuka sisi sote tulilelewa katika mapenzi hayohayo mpaka tumefikia kuwa watu wazima, halafu tunamwona mwanamke aliyeko ndani hafai sababu za msingi hakuna visingizio vingi. Inakumbushwa sisi wanaume ni viongozi wa nyumba sasa mkeo mtoto akikosea kama hatutatumia busara kumelimisha tutumie mabavu huo utakuwa si utawala sasa tubadilike tuwaheshimu mama zetu wake zetu. Kwani tumelelewa katika mazingira magumu sana.