Posts

Showing posts from May 7, 2010

MIHOGO YAFUMUKA

Image
Ndugu zangu nafikiri sisi waafrika hakuna asiyelifahamu hili zao maalum la mhogo kwani imekuwa ni chakula cha wakati mgumu hata kama mvua zitaacha kunyesha kwa kipindi fulani hili zao linavumilia, Sasa dhumuni la kukuwekea kitafunwa hiki ni ujitahidi kama una eneo hata la mita tatu katika nyumbani kwako upande japo mashina mawili. usibweteke panda halafu utaukumbuka ujumbe huu.

VIJANA SASA WAAMUA WAMECHOKA

Image
Ni baada ya kijana huyu ambaye amezunguka baadhi ya mikoa ya hapa Tanzania katika kutafuta ridhiki na hata hivyo siku moja katika mizunguko yake ya maisha alikutana naye kimwana mrembo na kuchukua uamuzi wa kufunga naye ndoa kama inavyoonekana katika picha. Napenda kumpongeza kijana huyu kwa sababu tendo la kuoa kwa vijana waliowengi limekuwa ni jambo gumu sana wakijisindikizia msemo wao wa unaoa usiku asubuhi unaacha kuishi na mke kazi. sijajua wanaogopa ugumu wa maisha au kupigwa na wake zao. Vijana huu ndiyo wakati wenu wa kujipa changamoto ya maisha iga mfano wa huyo kijana hapo juu.

FURAHA YA WATANZANIA

Image
Kulia kwako msomaji ni Rais waJamhuri ya muungano wa Tanzania na kushoto kwako ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, wakiwa wamefurahi.

JE MARADHI AMBUKIZI YA UKIMWI YATAKWISHA

Image
Imekuwa ni kawaida kwa maeneo yenye hali ya joto baadhi ya wanawake kuvaa nguo nyepesi lakini kwa hivi sasa imekuwa ni kukomoana, kwani mwangalieni huyo dada vizuri kila kona na munieleze je tutafika,zunguka maeneo ya mkoa wa mbeya ni moja ya sehemu zenye baridi lakini utawakuta kama hawa sijui ni joto au wanatatizo.Tujaribu kuchangia mada hii ili tuweze kuboresha maisha yetu na tuyakemee yale mabaya. mwandishi techniciani msofe.