Posts

MAAFALI YA CHUO KIKUU CHA MWALIMU NYERERE

Image
 Leo ilikuwa  ni furaha sana kwa bi Zena Mtengeti kwani ndo siku muhimu kwa ngazi ya kielimu kwani ndo siku yake ya kutunukiwa shahada ya kwanza ya Jinsia na Maendeleo ya jamii , watu kanza wa kaza walifika kwa ajili ya kumpongeza picha ya pili toka juu ni mume wa zena Mtengeti akimvisha taji kwa ishara ya kumpongeza mkewe na  kumhusia maneno yafuatayo mwanzo wa shahada ya kwanza iwe ni faida kwa Taifa lako, na uwe mwanzo wa shahada ya pili na akasema hongera sana!!!!!!!!!!!!!!.

BIBI AINI

Image
Huyu ni mama mzazi wa Said  Msofe akiwa na Mwali wake zamani wa mtoto wake wa pili wa kiume Salum msofe.

MWALIMU NYERERE MEMORIAL ACADEMY

Image
Wanafunzi hawa wakiwa na furaha ya kutosha kabisa wakiwa katika sherehe ya maulidi ya kuhitimisha mafunzo yao ya chuo yaliyoanza mwaka 2010 hadi 2013, baadhi ya picha anayekula aliyeweka nyama ya kuku mdomoni ni Zena Mtengeti, juu kabisa anayekutanzama na mwenye tabasam ni Sada Wakasi, anayeangalia kamera ni Fatuma.

Hot news

Image
Picha za Aini Msofe akiwa na umri wa miezi kumi kama unavyoona mtoto akiwa na tabasam la kutosha na mshangao wa mambo mbalimbali ya kidunia na pia anasikitika watu wa dunian na mambo yao. na kuona naye yupo duniani la msingi ni kuzidisha dua kwa mola wetu atusamehe.

HABARI NA MATUKIO

Image
Picha ya kwanzaa hapo juu ni ndugu Kibarua ambaye ni moja ya watu wenye utu na ubinaadamu hasa wakati wa shida, ndugu huyu aliweza kujitoa bila ya kujali ratiba zake nakusaidia pale ambapo shida ilijitokeza. Na picha ya mtoto hapo juu ni Aini msofe.

JIJI LETU

Image
Aini Msofe akiwa juu hapo na mama yake wakiwa sonara iliyoko Mlimani City, na chini ni picha na manjari ya jiji la Dar es salaam.

AINI MSOFE

Image
Picha za Aini msofe akiwa na mama yake, siku ya kwanza kupelekwa Mlimani City Shopright, kwa ajili ya kutoga(kutobolewa) masikio kwa ajili ya kuvaa hereni. Dada aliyevaa baibui ndiye mtoboaji masikio ni mtaalam  na ana uzoefu wa kutosha anapatikana Mlimani City ukifika Uliza kwa sonara wanakotoboa masikio.

MR S.M MSOFE

Image
                                                                       R.I.P, Mr S.M. Msofe   General Postamaster wa Tanzania Mstaafu, Alizaliwa mwaka 1948-2013 alipoiaga dunia, Tarehe 11-12-13 Nyumbani kwake Mapinga mkoa wa Pwani, Na amezikwa Tarehe 14-12-13 Nyumbani kwake mapinga. Alizikwa na mamia ya watu akiwemo Mkuu wa Posta wa sasa Mr mndeme. Mungu aiweke Roho ya Marehemu mahali Pema PEPONI AMINA.       Watu  wliohudhuria wakiwa na majonzi tele, kila mmoja akionesha masikitiko yake juu ya msiba wa marehemu, kwani alikuwa sio mtu mwenye kujisikia alikuwa ni mwenye usikivu kwa kila rika na hakuwa ...

MAISHA MAZURI

Mambo ya kuzingatia ili kuwa na maisha mazuri,  Unashauriwa kumchagua mwenzi wako ambaye mnapatana kwa kina na kupanga mambo endelevu ya kimaisha, pia kuacha  tamaa ya maisha.

ERASTO MSUYA

Image
Erasto Msuya auwawa kinyama Arusha, Hapo ni picha ya marehemu. hakika tutakujulisha kadri tutakavyopata taarifa, na maendeleo ya msiba mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi.

MAMA AINI

Image
Mama  Aini siku moja ikiwa ndo katoka kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya mwanae Aini Msofe, akiwa anajipatia vitu vya kuongeza vitamini.

AINI MSOFE

Image
Mtoto Aini Saidi msofe siku aliyofunguliwa jalada la mahudhurio clinic ya watoto GMH mwenge Aini Msofe alizaliwa akiwa na uzito wa kg 3.6 na leo amefikia uzito wa kg 5.6 pia ameweza kupatiwa chanjo ya sindano mbili za mapaja, na matone mdomoni.

AINI SAIDI MSOFE

Image
Historia ya Aini Said Msofe, amezaliwa Tarehe 7 Jun 2013 siku ya ijumaa saa 3:56 alaasiri katika Hospital ya Lugalo(GMH). Nakurejea nyumbani siku ya jumapili ya Tarehe 9 jun 2013 saa 12:03 mchana, Chanjo ya mtoto kwa mara ya kwanza baada ya kuzaliwa aliipata katika hospital  ya mwananyamala siku ya jumatatu ambapo alipata matone tu, na siku ya Ijumaa jun 2013 alipata chanjo ya sindano katika Zahanati ya Kambangwa iliyopo  mwananyamala karibu na  hospital kuu ya mwananyamala, kabla sijaenda mbali na histori hii shukurani a dhati zimuendee DR Mwanasali na wengine katika kufanikisha uzao wa mtoto AINI SAIDI MSOFE.